Mtaani Mambasa jimboni Ituri vijini tano vimeshambuliwa na wahuni wa ADF kwa mda wa juma moja hata kusababisha watu kumi na sita kuuliwa na wengine wengi wakiwemo Watoto kutekwanyara. Shirika la raia laomba kwa serkali kuzidisha msako zidi ya waasi hawa.
Huko Kananga Watumiaji wasimu ya mikononi wataabika kwa kuongezeka kwa garama ya mawasiliano, lakini piya mtandao usiyo kuwa taratibu
Mjini Kolwezi, kazi ya ukarabati wa kilometa sabini na tano ya barabara yaizinishwa rasmi, huko, viongozi wakipangilia kueneza kilometa mia mbili ya barabara mjini mjini huko.






