" Kazi ya baraza la bunge ni gani ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” KAZI YA BARAZA LA BUNGE NI GANI ”

* Karne Kakasi,baraza la bunge ni chumba ao shina ya sheria za serkali. Kazi yake ni kuunda na sheria muhimu kwa uongozo wa vituo vya inchi.Kufatana na sheria mia moja ya katiba ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, baraza la abunge linachagua sheria, linachungua mwenendo wa serkali, wa makampuni ya serkali na pia viwanda na kazi za serkali.
Katika ainchi yaetu,baraza la bunge inayo vyumba mbili.Chumba kidogo yaani wakisema akatikalugha la kifransa chambre basse inayaoitwa bunge la taifa, na chumba kikuu yaani chambra haute- Senat, wakisema katika lugha la kifransa, baraza la wazee wa bunge. Kila chumba kinacho uongozo wake wa kipekee, na mfuko wake wa pesa kwa uongozo wa kazi zake.
Wanamemba wa bunge la taifa wanaitwa wateule wa bunge la taifa yaani wa députés nationaux katika lugha la kifransa., na wale wa baraza la wazee wa bunge wanaitwa wazee wa baraza la bunge yaani wa senateurs katika lugha la kifransa.

” NAMANA GANI HUENDA KUTIA KANDIDENTI KWA KUWA MWANAMEMBA WA BARAZA LA BUNGE ”

* Wakandidenti kwa kuchaguliwa kwa baraza la bunge wanajulishwa na vyama vya siasa ao vikundi vya siasa.
Wateule wa taifa ni wasimamizi wa rahiya na wanachaguliwa na rahiya katika hali ya siri.Wazee wa baraza la abunge wakiwa na madaraka ya taifa, wanasimamia jimbo. Waanachaguliwa kwa mzunguko wa pili na mabaraza ya majimbo.
Waateule wa taifa yaani wadeputes na wazee wa baraza la bunge wanacahaguliwqa pamoja na wamakamu wao mbili amabao wanaweza kuwagomboa, kufataana ana na oda iliyotiliwa, wakati wa kifo, kuacha kazi, kuwa na kizuhizo ao kufungwqa. Kufatana na sheria sifuru sita kistari sifuru sifuru ya tarehe kenda mwezi watatu mwaka waelfu mbili na sita,yenyi kuelekea uongozo wa uchaguzi wa auraisi ,wa wanabunge la taifa na alile la amajimbo, miji mikuu, na alaokaliti,mda wa kuchukua madaraka ya kazi kwa wanabunge na kwa wazee wa baraza unaanzishwa wakati wanakubaliwa na vyumba mbili vya baraza la bunge,na madaraka yao yanamalizika wakati baraza la bunge lipya linashimikwarnWateule wa taifa na wazee wa baraza la bunge wanachauliwa kwa mda wa miaka mitano.ya kurudilia mara moja.Inafaa kujua kama maraisi wazamani wa jamuhuri waliochaguliwa ni wazee wa baraza la bunge mpaka kufa kwao.

” BASI HAKI YA WATEULE WA BUNGE NA YA WAZEE WA BARAZA LA BUNGE NI GANI ”

* Wateule wa ataifa na wazee wa baraza la abunge wanao haki ya kutembea inchoini kote bila hata tatizo moja na kuondoka nje ya ainchi pasipo pia tatizo, Wanao haki kwa pesa na madaraka inayowapa huru na heshima.Na hiyo huenda kupangwa kulingana na sheria yenyi kuelekea pesa za serkali.Wateule wa taifa na wazee wa baraza la bunge wanao pia haki kwa malipo yao wakati wanaondoka madarakani mwao , malipo ya mda wa miezi sitarnInafaa kujua kama mpango wa malipo hayo inalingana na sheria , na pia haki zingine za wanabunge zenyi kupangwa na sheria ya kila chumba cha baraza la bunge.

” KWA MWISHO TANAWEZA KUJUA WAKATI GANI MDA WA MADARA YA WATEULE WA TAIFA NA ULE WA WAZEE WA BARAZA LA BUNGE UNAMALIZIKA ”

* Mda wa madaraka ya wateule wa taifa na ya wazee wa baraza la bunge unamalizika wakati mda wa bunge unamalizika, wakati wa kifo, wakati wanajiondosha kazini, ao wakati wanao kizuizo mpaka mwisho, wakati wa ukosefu wa nguvu ya kutumika, kutohuzuria kunako mikutano mda mrefu pasipo ruhusa zaidi ya mikutano inne kwa kila kipindi,kufukuzwa kulingana na sheria kuhusu uchaguzi,kuitika kazi ingine isiyo lingana na mwanabunge ao mzee wa baraza la bunge,ao kufungwa kulingana na kosa lenyi kutendwa kwa kusudi.
Inafaa tujue kama kila mteule wa taifa ao mzee wa baraza la bunge mwenyi anaondoka katika chama chake cha siasa ni wakati baraza la bunge lingali na madaraka, huyo anapashwa pia kuacha kazi ya mteule wa taifa ao mzee wa baraza la bunge,kwani hali ile aliipewa kutokana na chama chake cha siasa.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes CourtesrnTél. : 00243998909787rnE-mail : [email protected] [email protected] Swahili de DUNIA MUKUNDA