" Kazi ya baraza la bunge la jimbo ni gani na namna gani inapangwa ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” KAZI YA BARAZA LA BUNGE LA JIMBO NI GANI NA NAMNA GANI INAPANGWA “.

* Karine ulizo lako ni nzuri sana.Nukta ya 197 ya katiba ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, inajulisha kama bunge la jimbo ni kituo ao chumba cha uchunguzi wa jimbo.Chumba hicho kinachungua, kufatana na madaraka yenyi kuelekea jimbo, na kuchungua pia mwenendo wa serkali ya jimbo na kazi zake zingine. Wanamemba wa bunge la jimbo wanaitwa wateule wa bunge la jimbo.
Wanachaguliwa kwa kura ya uwingi na kwa siri ao kwa njia ya kuitwa ao kutajwa,kwa mda wa miaka mitano, ya akurudilia mara moja.
Kutana na nukta ya 143 na ya 145 ya sheria sifuru ,kistari sita, sifuru sifuru sita ya tarehe kenda mwezi wa tatu mwaka tunaorn kuhusu matayarisho ya uchaguzi mbali mbali, ya uraisi, ya wateule wa baraza la bunge la taifa, na lile la majimbo, wa miji mikubwa, komini na malokaliti, eneo la uchaguzi kwa wteule wamajimbi ni katika jimbo,mji na teritoria.
Katika mji wa Kinshasa ni komini.
Idadi ya viti vyenyi kukubaliwa kwa bunge la jimbo nirn-wateule 48 kwa majimbo yenyi kuwa na wachaguzi kati ya milioni mbili na elfu mia tano.
-wateule 42 wa majimbo yeni kuwa na wachaguzi kati ya milioni mbili na moja hadi milioni mbili na elfu mia tano.
-wateule 36 wa majimbo yenyi kuwa na wachaguzi kati milioni moja na elfu mia tano hadi milioni mbili ya wachaguzi.waliojiandikisha.
wateule 30 wa majimbo yenyi kuwa na wacahaguzi milioni moja na moja hadi wacahaguzi milioni moja na elfu mia tano.
-wateule 24 wa majimbo yenyi kuwa na wacahaguzi elfu mia tano hadi milioni moja.
wateule 18 wa majimbo yenyi kuwa na wachaguzi wenyi kuandikwa elfu mia tano ao chini ya idadi hiyo.

” KUNAKO SHURTI GANI KWA KUCHAGULIWA WATEULE WA MAJIMBO ? “rn rn* Karine, nukta 148 na ile ya 149 ya sheria kuhusu uchaguzi , zinajulisha kama daftari ya awakandidenti kwa mabaraza ya majimbo inajulishwa na vyama vya siasa ao makundi ya siasa. Wakandidenti wasiokuwa na vyama vya siasa yaani wakandidenti huru, wanajijulisha wenyewe,binafsi.Inafaa tuwakumbushe kama mkandidenti kwa baraza la bunge la jimbornanapashwa kutimiza mashurti hayo.
-awe mkongamanirn- awe na umri wa miaka 25 ya kuenea wakati anapotia kandidenti yake.
- awe na uhuru wa haki zake za kirahiya na za kisiasa rn- awe na ahali ya amchaguzi ao ajijulishe na kujiandikisha wakati anapotia kandidenti yake.Inafaa kujua kama wakandidenti kwa baraza la bunge la jimbo wanajijulisha kunako chumba cha Cei cha majimbo yao,kwa akutoa maoani yao.Maoni hiyo ya wakandidenti yanapashwa kuwa narn- barau inayofata hali ya barua ya CEI na inayosahiliwa na mkandidenti binafsi. Barua hiyo huenda kujulisha kama yeye kandidenti alikubaliwa na chama chake.
-cheti cha kujitambulisha chenyi kujulisha maisha yake mkandidenti.
– picha ndogo inne yaani photopasseports.
sura ao alama ya chama cha siasa ao ya akundi lake la siasa- majina ya wamakamu wake mbili

” UMBALI MBALI NA SHURTI ZILE,KANDIDENTI KWA BARAZA LA BUNGE JIMBONI ANAPSHWA KULETA TENA NINI.”

* Karine, swalilako ni nzuri sana. Kwani inafaa kujua kama kandidenti anapshwa kuongeza umbali mbali na maoni yake vitu hivyorn- sura ya cheti chake cha mchaguzirn -cheti chake cha kuzaliwarn -karatasi yenyi kujulisha kama kandidenti ao daftari ya wakandidenti ililipa pesa zenyi kuombwa , dola za kimarekani makumi matano ,pesa ambazo huenda kutiliwa kunako sanduku ya serkali,siyo za kurudishia kandidenti kwa mwisho.
-barua ya akujulisha kama chama cha siasa ao kundi la siasa la akandidenti lilikubali awe mkandidenti.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes CourtesrnTél. : 00243998909787rnE-mail : [email protected] [email protected]

Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA