" Watu wengi hujiuliza kama franka iliyolipwa na kuombwa na Cei kwa wakandidenti kwa uchaguzi mbali mbali itatumiwa namna gani ? " .

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” Watu wengi hujiuliza kama franka iliyolipwa na kuombwa na Cei kwa wakandidenti kwa uchaguzi mbali mbali itatumiwa namna gani ? ”

Karine ,,kwanza namipia nakusalimu.Shurti ya kwanza ya amuhimu kwa uchaguzi huru, wakweli na wakukamilika ni sherti uchaguzi ule uwe wa kugombea.Karine , ndio maana uchaguzi wa namna ile inafaa uwe na wakandidenti wengi wakuugombea.ili wachaguzirn wapewe bahati na kujichaguliya wanaostahili..
Shurti za kuwa kandidentio huenda kusawishi idadi ya wakandidenti.
Kwa jumla,zaidi shurti zile ni nyepesi, zaidi kunapatikana wakandidenti wengi wenyi kujiandikisha.Lakini inafaa kujua Karine na kujiuliza swali lenyi kuelekeya kama, wakandidenti ngapi wanaweza kupatikana wakati wakura moja.Kuweko kwa wakandidenti wadogo huenda kupunguza bahati ya wachaguzi.Lakini ikiwa kama idadi ya wakandidenti ni nyingi,zaidi rahiya wanakumbwa na magumu kwa kuchagua wakandidenti wa kweli.Katika jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Cei iliamuru kama hatua ya kuomba wakandidenti pesa za kulipa wakati wanatia dossiers zao kwa uchaguzi mbali mbalai ni mashindano makubwa.Franka zilizoombwa ni alama ya kutimiza shurti kwa uchaguzi.Ni kusema kama, pesa zile ni lupango yenyi kuonyesha kama kila kandidenti anahitaji kushiriki kwa uchaguzi ili agombee kiti na wengine.Kufatana na sheria sifuru , sita kistari, sifuru sifuru sita ya tarehe kenda mwaka wa 2006 yenyi kuelekea matayarishao ya uchaguzi mbali mbali katika jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo- uchaguzi unaoelekea uraisi wajamuhuri , ya wateule wa bunge la taifa na lile la majimbo, ya amiji mikubwa, komini na lokaliti. pesa zilizolipwa hazitarudishwa.ZILIINGIZWA KATIKA SANDUKU YA SERKALI.

” DUNIA MUKUNDA MILEMBA,TUNAWEZA KUJUA FRANKA ZAkONGO NGAPI AMBAZO KILA MKANDIDENTI KWA UCHAGUZI MBALI MBALI ALIPASHWA KULIPA ILI AKUBALIWE KAMA MKANDIDENTI INCHINI kONGO YA KIDEMOKRASIA ? “.

* Karine Kakasi,sherie kuhusu uchaguzi ni wazi juu ya jambo lile.Pesa zilizoombwa si sawa kwa kila daraja la uchaguzi. Kwa mfano,wakandidenti wote kwa uchaguzi wa uraisi wa jamuhuri walipashwa kulipa pesa yenyi kukadirishwa kwa franka za Kongo milioni makumi mbili na mbili,wakandidenti kwa bunge la taifa na wazee wa baraza la bunge la taifa walipshwa kulipa franka za Kongo elfu mia moja na kumi, wanabunge la majimbo walipashwa kulipa franka za Kongo. elfu makumi tano na tano. wakandidenti maliwali wa majimbo walipshwa kulipa franka za Kongo elfu mia sita makumi sita, wameya na makamu waoa ni elfu miaamoja na kumi, wabourgmestres na makamu wao ni elfu makumi munane na munane, na washauri wamiji mikubwa ni elfu makumimbili na tano.
Kwa upande wao, washauri wa makomini na wasultani wa sekta pamoja na makamu wao ni elfu makumi mbili na ambili.Kwa mwisho, washauri wa secteurs waanapashwa kulipa franka za Kongo elfu kumi.

” DUNIA MUKUNDA MILEMBA.KWA MWISHO , WASIKILIZAJI WETU WANATAMANI KUJUA KAMA FRANKA ZILE ZITAFALIA KWA NINI ? “.

* Karine, kufatana na maoni ya presidenti wa komisheni huru , mpadri Appolinaire Malu Malu, franka zile zitachungwa na uwaziri unausika na bageti ya serkali wakisema katika kifransa,ministere du budget, na huo uwaziri ndio huenda kuusika na ugawanyaji wa pesa zile katika kazi mbali mbali za serkali.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes CourtesrnTél. : 00243998909787rnExt. : 6961rnE-mail : [email protected] [email protected]

Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA