Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.
” Namna gani huenda kushimika katika madaraka yao wanamemba wa bunge la taifa na wazee wa baraza la bunge la taifa ? ”
* Karine KAKASI,kwa kujibu kwa ulizo lako inafaa kujua akama wanamemba wa bunge la taifa na wale wazee wa baraza la bunge wanachukua madaraka yao siku kumi na tano,kiisha kutajwa kwa nukta ao alama za uchaguzi ya waliogombea kuwa wateule wa bunge la taifa .Nukta 114 ya Katiba ya inchi na nukta 224 ya sheria, sifuru sita,kistari sifuru sifuru sita ya tarehe kenda mwezi wa tatu wa elfu mbili na sita, sheria yenyi kuhusika na matayarisho ya uchaguzi mbali mbali,. ya uraisi wa jamuhuri , ya wateule wa bunge la taifa na lile la majimbo, ya miji mikubwa, ya makomomi na ya malokaliti kataika eneo lote la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, sheria ile inahakikisha kama kila chumba cha bunge la taifa kinakusanya wanamemba wake kwa mkutano usio wakawaida ,kiisha siku 15 tangu kutangazwa kwa nukta za kura, na hiyo ni kwa shabaa ya kushimika madarakani chumba cha mda,kitakacho ongozwa na mmoja wa wateule mwenyi kuwa na mika nyingi, na huyo atasaidiwa na wanamemba mbili wenyi kuwa na miaka ya chini kuliko wengine.Chumba kile cha mda kitajiandaa kwa hatua ya kukubali madaraka ya wateule wa bunge la taifa wenyi kuwa katika kila chumba, pia chumba kile kulingana na uchaguzi kitajiandaa kwa kushimika chumba kamilifu. Na chumba kile kamilifu kitajiandaa kwa utungo wa mipango yenyi kuelekea uongozo wachumba. Karine Kakasi ,inafaa kujua kama mkutano ule usio wa halali huenda kumalizika wakati nukta zote kuhusu maoni ya wateule iliyostahili kuchunguliwa inachunguzwa.
” Basi bwana Dunia Mukunda Milemba,tunaweza kujua kama ni wa nani wenyi kuunda kila chumba cha bunge ? ”
* Naam , Karine KaKasi,kila chumba cha kila baraza la bunge kinaundwa na presidenti,akiwa na wamakamu wake mbili, mwandikaji mmoja na makamu wake mmoja, questeur mmoja akiwa pia na makamu wake mmoja.
Uchaguzi ao kutajwa kwa wanamemba wa chumba kamilifu cha chumba cha kila tawi ao chumba cha bunge,kinalazimishwa kuchungua usawa kati ya wanamemba wanaume na wanawake.Chumba cha mda kinapoteza madaraka yake mara hapo chumba cha kamilifu kinashimikwa.Uchaguzi wa wanamemba wa chumba kamilifu unafanyika mbele ya wanamemba wote na ni uchaguzi unaofanyika katika siri kwa kura ya mwenyi kupata sauti nyingi.
Kwa ukumbusho tutawajulishe kama baraza la bunge la taifa ni kiuongo cha bunge la taifa.Baraza la bunge la taifa linalo kazi ya kuandika nukta kuhusu maoni ao mipango huenda kusaidia kwa uongozo wa vituo vya inchi.Kufatana na nukta 100 ya Katiba ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, bunge la taifa linachagua sheria ilyotungwa, bunge la taifa linachungua kazi za serkali, makampuni ya serkali na pia mashirika na kazi za serkali.Katika inchi yetu , jamuhuri ya kidemorasia ya Kongo. baraza la bunge la taifa ni lenyi kuundwa na vyumba mbili: chumba cha chini chenyi kuitwa baraza la bunge la taifa yaani ASSEMBLEE NATIONALE ,wakisema katika lughja la kifransa. Chumba kikuu kinachoitwa baraza la wazee wa bunge,yaani katika kifransa SENAT.Kila chumba kinacho uongozo wake wa kipekee na pia uongozo wake wa kifeza.
Wanamemba wa baraza la bunge la taifa wanaitwa wateule wa bunge yaani DEPUTES NATIONAUX katika lugha la kifransa., na wanamemba wa baraza la wazee wa bunge wanaitwa wazee wa bunge la taifa.Karine Kakasi ,inafaa kujua kama presidenti wa baraza la wazee wa bunge la taifa anapashwa kuwa mkongomani wa tangu kizalikiyo.
Texte de SAMUEL KATSHAK rnOndes courtes 3è HeuresrnTél. : 00243998909787rnExt. : 6961rnE-mail : [email protected] [email protected]
Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA







