" Namna gani utetezi wa kura ya mzungukuko wa pili kwa uraisi wa jamuhuri huenda kufanyika,pia ule wa wakandidenti kwa bunge la majimbo ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” Namana gani utetezi wa kura ya mzungukuko wa pili kwa uraisi wa jamuhuri huenda kufanyika,pia ule wa wakandidenti kwa bunge la majimbo ? “rn rn* Karine Kakasi, kwa ukumbusho kuhusu swalilako, inafaa tujulishe kama utetezi wa uchaguzi ni wakati unaotangulia uchaguzi wenyewe.Ni wakati ambako vyama vya siasa na wa kandidenti, wanajitetea, ni kusema wanajulisha mipango yao ya siasa na uzuri wa kazi watakaoifanya kwa manufaa ya rahiya, kwa lengo lakupata sauti nyingi za wachaguzi.Lakini, inafaa kutafautisha utetezi kiserkakli wa uchaguzi na autetezi wa uchaguzi kwa usikivu wake kwa jumla.
Utetezi kiserkali wa uchaguzi ni mda ambao wakandidenti na vyama vya siasa wanajieleza kupitia vituo vya upashaji wa habari Redio, televisieni na magazeti kufatana na sheria kiserkali yenyi kuelekea uchaguzi.Wakandidenti wote wanapashwa kupewa mda sawa kwa kujieleza njiani mwa anga kupitia redio ,televisiene. Katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo ni Haute Autorite des medias ndio inayo madaraka ya kuchungua kama sheria ile inaheshimiwa.Kuhusu uchaguzi wa wateule wa baraza la mabunge majimboni, Cei iliweza kuchukua hatua ya kuchukua siku 30 kama vile mda kiserkali wa utetezia . Ni tangu tarehe 28 mwezi wa kenda hadi tarehe 27 mwezi wa kumi mwaka huo wa 2006 pa saa sita ya usiku.Na hatua hiyo inafatana na nukta ya 28 ya sheria sifuru,sita,kistari, sifuru ya tarehe kenda mwezi wa tatu mwaka wa 2006, sheria yenyi kuelekea matayarisho ya uchaguzi mbali mbali ya uraisi wa jamuhuri, ya wana bunge la taifa,lile la majimbo, uchaguzi wa miji mikubwa, komini na lokaliti ,katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo. Cei iliweza pia kushimika mpango kuhusu uchaguzi wa uraisi wa jamuhuri kwa mzunguko wa pili ,tarehe 29 oktoba mwaka tunao na ni tarehe hiyo hiyo ndipo kutafanyika pia uchaguzi wa wateule wa mabaraza ya mabunge ya majimbo.Kuanzishwa kiserkali kwa mda wa utetezi wa uchaguzi wa raisi wa jamuhuri kwa mzunguko wa pili. ulipangwa kupitika mda wa siku 15, ninkusema tangu tarehe 13 oktoba pa saa sita ya usiku hadi tarehe 27 oktoba mwaka tunao ,pa sa sita ya usiku.
Utetezi wa uchaguzi kwa kufatana na maoni mengi, unajulisha mda ambao vyama vya siasa na wakandidenti wanajijulisha na kujulisha pia maoni yao na mipango yao. Wakati huo si wakati wa utetezi ao kampenyi yenyi kuchunguzwa na sheria kuhusu uchaguzi, basi tuseme kama ni wakati wauhimizaji.Kwa upande ungine, hatua zote zenyi kuelekea sheria ya kuhazibu ao katiba yenyi kuelekea ulinzi wa heshima ya mtu,kutomsemea mwengine uwongo,kusema maoni ya chuki, ya akuharibu heshima ya wengine, kusema maoni ya ubaguzi wa makabila, sheria zenyi kukataza maoni yale ,sherie zile zinapashwa kuheshimiwa.Vyama vya siasa na wakandidenti wanapashwa kutii mipango kuhusu mwenendo bora wa uchaguzi,mipango waliohisahihi kuhusu uchaguzi mbali mbali.

” Basi, Dunia Mukunda Milemba. ni nani anayepashwa kufanya utetezi wa uchaguzi na namna gani utetezi ule huenda kufanyika ? ”

* Karynne Kakasi, unajua kamasheria kuhusu uchaguzi inampatia kuila kandidenti ao kila chama cha siasa kufanya utetezi wake mda uliopangwa na sheria.Nukta 29 ya sheria kuhusu uchaguzi inahakikisha kama mikutano ya uchaguzi inafanyika kufatana na mipango yenyi kuelekea mikutano ya watu wote. Na mikutano ile inatayarishwa na vyanma vya siasa na wakandidenti huru, wasio na vyama vya siasa..Mikutano ya utetezi kiserkali wa uchaguzi mbali mbali yanafanyika kwa uhuru katika eneo lote la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo,lakini inafaa walioanda mikutano yenyeweao maandamano yale wajulishe kwa njia ya barua kiongozi wa serkali saa 24 mbele ya kuanzishwa kwa mikutano yao ao maandamano ya watu wote. Walioandaa mikutano ile wanalazimishwa kuchungua mwenendo yao, ili waandamanaji ao walioshiriki katika mikutano wasije wakaharibu hali ya usalama kwa wote na kama wanatiii sheria. Wakati huo , kutia picha mahali pa wazi, ao matangazo na sura ya wakandindenti inaruhusiwa kataka hali iliyojulishwa na Cei. Lakini, kupandika picha ao matangazo ya utetezi kunako vyumba vya serkali kunakatazwa.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes courtesrnTél. : 00243998909787rnExt. 6961rnE-mail : [email protected] [email protected]

Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA