Siku ya tatu mjini Kinshasa, hakukua na msongamano wa magari kwenye barabara kuu kadhaa kama kawaida mjini humo. Ni kutokana na wito wa upinzani kwa mgomo wa jumla ili kupinga mabadiliko yoyote ya Katiba.
Katika jimbo la Tshopo, boti iliyo kuwa ikiwabeba abiria na mizigo ilipinduka siku ya pili kwenye Mto Aruwimi, katika mtaa wa Banalia. Hadi sasa, zaidi ya watu sitini walio kua humo hawaja patikana.
·Na jimboni Kivu kaskazini, watu kumi na sita waliuawa, wengine watano hawajulinake walipo, na nyumba kadhaa na pikipiki kuungizwa: hayo yalitokea katika shambilizi la waasi wa ADF katika usiku wa kuamkia hii siku ya tatu Huko mtaani Beni.





