Habari za Asubui, siku ya pili 02 juni 2026

Kutokana na Ebola huko Ituri, Serikali ya Kongo na Shirika la Afya Duniani wamehakikisha juhudi zao ajili ya kulinda afya ya watu. Ndio maana wametangaza kuzidisha kazi zao ili kukomesha magonjwa haya haraka iwezekanavyo.

Kumeripotiwa ajali  mpya ya meli siku ya sita, kwenye Mto Kwilu. Ajali hiyo ilisababisha  vifo vya watu kumi na moja. Hadi sasa, zaidi ya abiria hamsini hawajulikani walipo.

Katika mpango wa kupambana na usafirishaji haramu wa kasuku jimboni Maniema, Shirikisho la Lukuru, liliwaachilia zaidi ya kasuku arobaini wa kijivu ili warudi katika makazi yao ya asili.

/sites/default/files/2026-06/02062026_-_jp_sw_-_matin.mp3