Wafanyakazi wanne wa shirika la msalaba Mwekundu walijeruhiwa vibaya siku ya kwanza mjini Bunia. Ilikua walipo endesha maziko salama ya mtu aliye fariki kutokana na Ebola, ndipo walishambuliwa na vijana waliotaka kufungua jeneza kwa nguvu.
uwepo wa wafugaji wa Mbororo kaskazini-magharibi mwa DRC ulikuwa kiini cha majadiliano siku ya kwanza katika Bunge la Kitaifa. Huko, Naibu Waziri Mkuu Guy Kabombo, anayesimamia Ulinzi wa Taifa, alikua mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la taifa.
Jimboni Lualaba: Wafanyakazi wa Tenke Fungurume Mining waendelea na mgomo wao, huku wakiomba kuboreshwa kwa mishahara yao ya msingi na mazingira ya kazi.
/sites/default/files/2026-06/03062026_-_jp_sw_-_matin_-_ok.mp3





