Watu watano walio zaniwa kuwa na ugonjwa wa ebola katika gereza kuu la Bunia, baada ya vipimo walionekana kuwa hawana ugonjwa huo. Ila, hatua za kuweza kujikinga zina endelea kuchukuliwa.
Na jeshi la taifa, Fardc kupitia msemaji wake limeweza kutoa siku ya tatu taarifa kuhusu maendeleo ya hali ya usalama inchini Congo.
Mjini Kinshasa, bunge la taifa limeweza kupitisha pendekezo la sheria kuhusu wapangaji na wenyeji nyumba, hasa zile ambazo si za wafanya biashara.
/sites/default/files/2026-06/0806026-p-sw-journal_swahili-de_ce_lundi_matin-00.mp3






