Maaskofu wa kanisa la katolika wameweza kutoa msimamo wao kuhusu hali ya inchi ya jamuhuri ya kidemocratia ya Congo. Hiyo, ni baada ya mkutano ambamo waliweza kujadili maswala mbalimbali ambayo yanahusu taifa la Congo.
Watu sita walio pona ugonjwa wa Ebola waliweza kuondoka hospitalini mbele ya ujumbe wa serkali ulio weza kutoka mjini Kinshasa ; na serkali imekua ikiwaita raiya kuweza kujikinga ili kuweza kushinda ugonjwa huo wa Ebola.
Pa Kananga, bei ya samaki ina endelea kupanda kutokana na hali ya usafiri ambao wachuuzi wanakua wakiuchukua siku hizi, na garama ya maisha ya watu wenye pato ndogo ndio wanaendelea kuangamia.
/sites/default/files/2026-06/2206026_-_jp_sw_-_lundi_matin_-_00.mp3





