Journal matin

Habari za siku ya tano asubuhi tarehe 15/12/2023

  • Ceni ilizindua jana siku ya inne  kutoka Kinshasa awamu ya mwisho ya mafunzo  ya wafanyakazi  wa uchaguzi ambao watafanya shughuli za uchaguzi na kuhesabu kura siku ya tatu ijayo .
  • Siku chache  kabla ya uchaguzi, mahitaji ya  vieti via uchaguzi yamekuwa mengi huku huduma ya utoaji ni ngumu sana, wanalalamika baadhi ya wachaguzi  ambao wakati mwingine hulazimika kusubiri kwa zaidi ya wiki moja ili kupata cheti hicho.
  • Vietu vietu via uchaguzi viote havisomeki, na si mara zote tumeweza kupata  vingine kutoka CENI. Tutafanya dje ili kuchaguwa  wagombea wetu katika uchaguzi wa pamoja uliopangwa kufanyika tarehe makumi mbili mwezi huu?? Hivi ndivyo wanavyoshangaa wakazi kadhaa wa mji wa Bandundu katika jimbo la Kwilu.
  • Jimboni Kivu ya Kusini, katibu mkuu jimboni   ya CENI anahakikisha kuhusu maendeleo mazuri ya mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo.
  • Katika jimbo la Tshopo, chini ya wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Kongo , kiongozi kuu ya CENI jimboni  anasema tayari wamesambaza zaidi ya asilimia makumi  kenda na tano ya vifaa vya uchaguzi katika eneo lote.
  • Huko Ituri, kampeni ya uchaguzi ni ya kutisha sana katika usulutani wa Banyari Tchabi na  maeneo mengine vingine jirani kusini mwa Irumu.
  • Tume ya Maaskofu ya Haki na Amani ya Jimbo Kuu la Lubumbashi inafanya kampeni kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi wa amani.
  • Katika jimbo Ituri, zaidi ya hekta elfu nne na mia tano za mazao ya mchele na mimeya mingine , viazi na mboga nyingine zimeharibiwa tangu siku ya pili na mafuriko ya Ziwa Albert katika  mtaa wa Djugu./sites/default/files/2023-12/151223-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3