Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi  tarehe 04/04/2023

  • Huko jimboni Kivu ya Kusini ambako   kisa kingine cha ajali  kilihesabiwa  kwenye Ziwa Kivu na kusababisha vifo na watu kupotea. Tukio hilo limetokea usiku wa tarehe mbili  hadi tarehe tatu mwezi wa inne mwaka huu tunao katika mtaa wa Idjwi.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, karibu watu makumi  mbili walikufa katika maporomoko ya udongo  jana  siku ya mungu  huko Bulwa, katika eneo la  Buabo mtaani  Masisi.
  • Katika jimbo la Sankuru, wanawake sita  walikufa na wengine inne kujeruhiwa vibaya, hii ni matokeo  ya maporomoko ya udongo yaliyotokea Jumapili katika  eneo la  Telecom katika mtaani  Kabondo huko Lusambo.
  • Kuliandaliwa Siku bila teksi za pikipiki siku ya kwanza hii katika mji wa Muanda jimboni Kongo Central . 
  • Katika jimbo la Tshopo,  kazi za majengo  kuhusu  mradi wa maendeleo wa mitaa  mia moja na makumi ine  na tano zilizinduliwa mwishoni mwa wiki hii huko Isangi, mji mkuu  wa mtaa wa Isangi  inaopatikana kwenyi  kilomita mia moja makumi mbili na tano na mji wa Kisangani .
  • Katika Jimbo la Tanganyika,  mgogoro wa mpaka unapinga eneo la Kalemie na lile la Nyunzu.Sababu ya mzozo huu ni , ugunduzi wiki chache zilizopita wa amana ya Coltan katika kijiji cha Sango Mutosha kilichoko kwenye mpaka kati ya maeneo hayo mawili.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, vikosi  vya Wanajeshi  wa Sudan ya Kusini viliwasili Goma siku ya mungu na siku ya kwanza hii , ili kuimarisha nguvu ya jeshi la EAC.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini,   kujiondoa kwa waasi wa M23, tangu siku ya mungu , kunathibitishwa na duru  kadhaa za eneo la Bambu. Hali hiyo hiyo huko  Kishishe, katika usuklutani wa Bwito, ambapo raia mia moja waliuawa mnamo  mwezi wa kumi na moja mwaka uliyopita.
  • Liwali makamu wa Jimbo la Ituri, Alongaboni  Benjamin, sasa ndiye mkuu mpya wa polisi wa kitaifa inchini Kongo ya Kidemokrasia ./sites/default/files/2023-04/04042023-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3