Journal Matin

Habari za siku ya tatu asubuhi tarehe 17/01/2024

  • Ni hii Leo siku ya tatu ndio imepita miaka makumi sita mitatu tangu Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice-Emery Lumumba kuuawa huko Élisabethville, jimboni Katanga 
  • Siku ya pili hii tarehe kumi na sita mwezi wa kwanza mwaka hu tunao inchi ya Kongo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka makumi mawili na tatu  ya kuuawa kwa Mzee Laurent-Desiré Kabila.
  • Kombe la Mataifa ya Afrika Huko inchini Cote d’Ivoire. Inchi ya Kongo yakidemokratia itacheza mechi yake ya kwanza siku ya tatu  hii na inchi ya Zambia. 
  • Msimamizi  wa Offisi ya Uchaguzi CENI mjini Kikwit katika jimbo la Kwilu amesimamishwa kazini na viongozi wake.
  • Huko Jimboni  Ituri, mkusanyiko wa jamii katika eneo la Irumu unahimiza vyama vya kisiasa vinaviopinga matoekeyo ya uchagzu ya wanabunge  kwenda ku mahakama ya kikatiba.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kusini, zaidi ya familia  mia mbili zimelala indje  kwa zaidi ya wiki mbili katika mtaa wa  Shabunda. 
  • Jimboni Kwilu, tarafa ya mazingira ya mkoa inasema imeona siku hizi  kuongezeka kwa  maji katika mito kadhaa na vijito vingine katika jimbo hilo. 
  • Tatizo la maji ya kunywa huko Mbuji-Mayi huko Kasai-Oriental. Vitongoji kadhaa vinavyotumiwa na shirika REGIDESO huko Mbuji Mayi vimekosa maji kwa karibu  wiki moja./sites/default/files/2024-01/170124-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3