Journal Matin

Habari z'asubuhi 11 Februari, 2025

  • Beni : Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa wa Kongo, Guy Kabombo Mwadiamvita, aliwasili jana siku ya kwanza huko Beni, mji mkuu wa muda wa jimbo la Kivu Kaskazini
  • Bukavu : Mahakama ya kijeshi ya Bukavu inasikiliza kuanzia hii siku ya kwanza kesi ya wanajeshi makumi nane na ine  wa FARDC wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya raia wasiopungua tisa huko Kavumu na Miti jimboni Kivu Kusini usiku wa kuamkia tarehe nane Februari mwaka tunao
  • Kinshasa : Ujumbe wa kutathmini na kufuatilia heshima ya haki za binadamu na wafanyakazi wa polisi umetumwa kuanzia jana siku ya kwanza tarehe kumi Februari, mjini Kinshasa na majimbo yote ambako Inspekta Mkuu wa Polisi iko./sites/default/files/2025-02/110225-p-sw-journalswahilimatin-00-web.mp3