Habari z'asubuhi 05 Mei, 2025
- Kinshasa : Chama cha Front Commun pour le Congo, FCC kwa ufupi, kinasema kinakerwa kufuatana na tangazo la Waziri wa Sheria kuomba Haki ya Kijeshi kuanzisha kesi dhidi ya kiongozi wake, Rais wa zamani, Joseph Kabila Kabange. FCC inaeleza kwamba huo ni udikteta
- Kinshasa : Shirika la Journaliste en Danger, linaomba kukomeshwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Muungano wa AFC-M23. Lilisema hayo siku ya sita tarehe tatu Mei, siku ya kuadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
- Kalemie : Huko Kalemie, zaidi ya visa mia moja vya kipindupindu, vikiwemo vifo viwili, vimerekodiwa tangu mwanzoni mwa wiki hii katika mitaa miwili ya afya ya Nyemba na Kalemie. Viongozi wa afya ndo wanatoa habari hiyo./sites/default/files/2025-05/050525-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3