Habari z'asubuhi 03 Juni, 2025
- Kinshasa : Mpinzani Martin Fayulu anapendekeza mazungumzo na kuongezeka kwa heshima na uwajibikaji ili kutatua suala la ukosefu wa usalama mashariki mwa Kongo. Alisema hayo katika hotuba yake hii siku ya kwanza mjini Kinshasa. Ombi ambalo rais wa jamuhuri Felix Tshisekedi anakubali, anasema msemaji wake
- Kinshasa : Miaka kumi na tano ya mauaji ya watetezi wa haki za binadamu Floribert Chebeya na Fidèle Bazana ilisherekewa hii siku ya kwanza tarehe mbili juni watetezi wa haki za binadamu wanaomba kesi ya mauaji hayo ifunguliwe upya
- Kinshasa : Mitihani ya serikali ya wanafunzi wa mwaka wa sita wa sekondari awamu ya makumi tano na tisa, kikao cha mwaka huu tunao, ilizinduliwa hii Siku ya kwanza kote inchini Kongo. Tunaizungumzia katika idhaa hii./sites/default/files/2025-06/030625-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3





