Journal Matin

Habari z'asubuhi 04 Juni, 2025

  • Kinshasa : Hotuba ya Martin Fayulu ni kitendo chenye umuhimu mkubwa wa kizalendo. Haya ni mameno ya msemaji wa serikali na wazieri wa mawasiliano na vyombo vya habari Patrick Muyaya. Alisema hayo hii siku ya kwanza wakati wa mkutano na waandishi wa ahabari akikaribisha mkono ulionyooshwa wa kiongozi wa upinzani Martin Fayulu kwa Mkuu wa Nchi Félix Tshisekedi
  • Bandundu : Zaidi ya shule nane  za serikali na binafsi zilihafribiwa kwa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni katika mji wa Bandundu, Makao Makuu ya Jimbo la Kwilu. Wanafunzi wamekosa kwa kufuatia masomo
  • Kinshasa : Mjini Kinshasa, wafanyakazi wa Ofisi ya Udhibiti wa Kongo (OCC) waliandamana hii siku ya pili tarehe tatu Juni, mbele ya makao makuu ya ofisi hiyo wakidai kuondoka kwa kamati ya sasa ya usimamizi. Kamati hiyo inatuhumiwa kwa makosa manne, yakiwemo usimamizi mbovu./sites/default/files/2025-06/040625-p-s-journalswahilimatin-00-web_0.mp3