Habari z'asubuhi 05 Juni, 2025
- Kinshasa : Shirika la Human Rights Watch linaripoti kwamba waasi wa M23, wakiungwa mkono na Rwanda, waliwaua takriban raia makumi mbili na moja huko Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini mwezi Februari. Akijibu ripoti hii, msemaji wa serikali alisema kwamba waasi hao wanaikalia Kivu Kaskazini kwa uhalifu
- Kinshasa : Wafanyakazi wa OCC ambao wako katika mgomo dhidi ya iongozi wao wanaitwa kuwa watulivu. Mkuu wa Ujumbe wa Muungano wa Kitaifa, Chiro Chiruza, anasema kwamba kazi ya kamati ya pamoja inafanyika ili kupata suluhisho kwa maombi yao
- Bunia : Huko Ituri, jamii jirani za wa Hema na wa Lendu za tabaka za Bedu Ezekere na Tambaki katika tarafa la Djugu zimeazimia kumaliza tofauti zao na kuishi pamoja kuanzia sasa. Mikutano hii iliandaliwa na sehemu ya Jinsia ya MONUSCO./sites/default/files/2025-06/050625-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3