Habari z'asubuhi, 16 Juni, 2025
- Kinshasa : Rais wa Jamuhuri Felix Tshisekedi anaomba maliwali wote wa Kongo wafanye huduma ya afya kwa wote kuwa kipaumbele cha kwanza katika majimbo yao. Alitoa pendekezo hili Siku ya tano huko Kolwezi jimboni Lualaba, wakati wa hotuba yake ya kufunga Kongamano la kumi na mbili la Maliwali
- Goma : "MONUSCO inasalia kuwa tayari kutoa msaada unaohitajika kwa nia ya kupata suluhu la amani kwa mgogoro wa sasa inchini Kongo. Ni maneno ya Bi Bintou Keita, mkuu wa MONUSCO aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari aliyouandaa mjini Goma siku ya tano
- Kinshasa : Mvua kubwa iliyonyesha katika jiji la Kinshasa siku ya sita asubuhi ilisababisha vifo, na uharibifu mkubwa wa mali. Profesa Kabasele Yenga Yenga, Mkuu wa Kituo cha Uchunguzi wa Anga kwa Maliasili na Hali ya Hewa, anashauri serikali kufikiria juu ya kutoa vifaa ili kukabiliana na athari mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa, kiafya na kibinadamu./sites/default/files/2025-06/160625-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3






