Habari z'asubuhi 23 Juni, 2025
- Kinshasa : Maaskofu wa kikatoliki wa Kongo wa CENCO na wale wa Kanisa la Kristo nchini Kongo, ECC, walimkabidhi Mkuu wa Nchi, jana Jumapili katika jiji la Umoja wa Afrika mjini Kinshasa, ripoti ya utume wao kuhusu mapatano ya kijamii, ambayo ni sehemu ya utafutaji wa amani katika eneo la Maziwa Makuu kwa ujumla, na hasa inchini Kongo
- Kinshasa : Shirika la sheria ya maendeleo ya kimataifa (IDLO) liliandaa siku ya tano mjini Kinshasa, mkutano wa Kujenga uwezo wa kitaaluma kwa ajili ya kukabiliana na rushwa nchini Kongo
- Bunia : Mjini Bubia, Monusco iliandaa siku ya tano mkutano kuhusu mapambano dhidi ya habari za uongo ambazo ni janga linalochangia kuendeleza mizozo ya kivita katika jimbo la Ituri./sites/default/files/2025-06/230625-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3