journal matin

Habari zetu za jumanne terehe 29 julay 2025.

  • zaidi ya milioni 1 ya wanafunzi wa segondari, wanahuzuriya tangu hii siku ya kwanza kwa Mtihani wa Serikali, toleo la 2025. Kati yao karibu asilimia 43 ya wasichana,Waziri wa Nchi anayesimamia Elimu ya Kitaifa, Raïssa Malu, alizindua rasmi mtihani huu katika shule ya Don Bosco la Masina.
  • "Acheni ushirikiano wowote na adui, kwa sababu ni vigumu kwa adui kufanya shambuliyo bila kupata msaada wa ndani." Wito mkali kutoka kwa Meja Jemadari Bruno Mandevu, Jumapili huko Komanda, ambapo zaidi ya raia 40 waliuawa na waasi wa ADF usiku wa Jumamosi hadi Jumapili.
  • Wizara wa Mazingira na Maendeleo uliandaa mkutano wenye kukusanya wataalamu katika niya ya kuboresha mipango wa Uratibu wa Mazingira na Maendeleo Endelevu wa Mkoa huko Matadi.

/sites/default/files/2025-07/29072025-journalswahilimatin00web.mp3