Habari zetu za jumanne tarehe 5 ogust 2025.
- 72% ndiyo kiwango cha ufaulu kwa mashindano ya serkali mwaka huu ndani ya majimbo ya elimu ya Kasaï Oriental 1, Haut-Katanga 1, na Kinshasa Mont Amba. Habari hii ilijulishwa na Wizara ya Elimu ya Kitaifa katika tangazo lake jumapili.
- karibu nyumba hamsini kuchomwa moto na raia wanne (04) waliuawa, akiwemo mwanamke na mtoto wake mchanga. Haya ni matokeo ya mapigano kati ya waasi wa AFC-M23 na wapiganaji wa Wazalendo wa kundi la APCLS.
- Idadi ya kesi za kipindupindu zilizo rekodiwa katika jimbo la Maniema ni kubwa, kulingana na ujumbe kutoka Wizara ya Afya ya Kitaifa na UNICEF. hali ya Maniema inatia wasiwasi mkubwa kwa viongozi wa serkali na washirika wao.
/sites/default/files/2025-08/05082025_-_journalswahilimatin-00web_.mp3