Habari zetu za ijumaa tarehe 29 Ogusti 2025.
- Bado kidogo kufunguliwa kwa mwaka wa shule Septemba 1, wazazi na wafanya biashara huko Goma wanasema kupitia matatizo makubwa ya kuwahudumia watoto wao. Sababu ni kwamba benki katika jiji la Goma zimefungwa tangu mwisho wa Januari.
- Mjini Boma katika jimbo la kongo ya kati:watu wawili waliuawa, wengine kadhaa kujeruhiwa, na gari ya polisi kuchomwa moto, na ofisi yake kuvamiwa. Haya ni matokeo ya mapigano kati ya wana polisi wa taifa na wakazi.
- Kasai-Kati, gavana alizindua rasmi usimamizi wa chanjo mpya ya malaria ya R21 kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 11. Joseph-Moïse Kambulu, alisifu juhudi ya pamoja ya kuwalinda walio hatarini zaidi, watoto, kutokana na malaria.
/sites/default/files/2025-08/290825-p-s-journalswahilimatin-00web.mp3