Habari zetu za Jumatano 10 september
- Volker Türk, kamisa mkuu wa Umoja wa Mataifa husika na Haki za Kibinadamu, anataja pande zote husika ndani ya vita, waasi wa M23 wenye kusaidiwa na jeshi la Rwanda. piya FARDC pamoja na wazalendo, wote wanahusika na kuongezeka kwa ghasia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini.
- Pale Lubero, raia karibu 70 waliuawa, karibu wengine 20 hawaja onekana, na vitu vingi kuharibishwa. hii ni matokeo ya shambulizi mapya ya ADF katika mji wa Ntoyo, kilomita 7 kutoka Manurejipa.
- Mwene Ditu, ubomoaji wa vibanda na nyumba zilizojengwa kinyume na sheria kwenye Barabara ya Kasa-Vubu uliendelea .operesheni inayolenga kuruhusu kuendeleya kwa kazi ya kupitisha maji safi ndani ya mgini.
/sites/default/files/2025-09/10092025-journaswahilimatin-00web_.mp3







