Habari zetu za Alhamisi tarehe 25 september 2025.
- Waziri wa Uchumi, Daniel Mukoko Samba, anahakikisha kama kushuka kwa bei yakubadili franka ya kongo zidhi ya dolla, ni matokeo ya juhudi za pamoja za serikali na Benki Kuu ya Kongo. Wiki iliyopita, dola moja ilikuwa na thamani ya franga 2,800 kwenye soko na Leo, inabadilika kwa 2,650 ama 2,700.
- "Operesheni za ulinzi wa amani zinakumbwa na kupunguzwa kwa bajeti na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa," Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, anayehusika na operesheni na ulinzi, Jumatano hii huko Beni.
- Kivu Kaskazini, mwaka wa shule wa 2025-2026 unakabiliwa na usumbufu mkubwa katika maeneo mbalimbali ya elimu katika jimbo zima. Katika mahali zimoja, shule hazija fungua milango tangu wiki tatu kabla ya kuanza kwa mwaka. Upande mwengine ni migomo ya walimu inayoendelea inazidi kuenea.
/sites/default/files/2025-09/25092025-journalswahilimatin-00web.mp3







