journal matin

Habari zetu za Jumatano tarehe 5 november 2025.

  • -Kinshasa: Hotuba ya Rais Tshisekedi mjini Doha.
  • -Goma: raia kadhaa walijeruhiwa katika mapigano kati ya AFC-M23 na CMC Nyatura huko Mashango, eneo la Rutshur.
  • -Kisangani: Kuwasilishwa kwa washukiwa 12 wa uhalifu
  • -Matadi: Waendesha pikipiki 25 kati ya 51 waliohukumiwa jana na Mahakama Kuu ya Matadi
  • -Bukavu: Uharibifu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Mwenga
  • -Kinshasa: Uharibifu wa mvua
  • -Goma: Malalamiko kutoka kwa Eneo la Afya ya Jamii ya Kibua katika eneo la Walikale kuhusu udhibiti wa magonjwa ya milipuko na milipuko.
  • -Mbuji-Mayi: Siku ya kwanza ya magonjwa ya akina mama na uzazi iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mbuji-Mayi.
  • -Kananga: Kuketi na wahudumu wa afya

2er partie : 

Mgeni Wetu ni : Bukavu: Shirikisho lenye lengo la kuendelesha urirhi wa hayati Askofu Christophe Munzihirwa, kupitia kuwahimiza watu kuishi pamoja kwa amani kati ya jamii, ilizinduliwa huko Bukavu tarehe 29 Oktoba, kumbukumbu ya miaka 29 ya kuuawa kwa askofu na askari wa AFDL. Mpango huu, unaoitwa Muungano wa Wananchi wa Mabadiliko ya Kijamii, ulifanya mkutano wa video na wanachama huko Goma, Kinshasa, Lyon (Ufaransa), na Brussels (Ubelgiji). Mratibu wa mpango huu ni Bi Alliance Heri, ambaye ni mgeni wetu akizungumza na Jean Kasami.
 
 
Ripoti:Jimboni Ituri, takriban watu mia moja, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, walipata huduma ya afya ya bure mjini Bunia siku ya ine iliyo pita. Hii ilifanyika wakati wa kampeni ya matibabu ya bure iliyoandaliwa na askari wa Monusco toka nchin ya Bangladesh. Lengo ni kuwalinda watu hawa kupitia huduma bora za afya. Ripoti MARTIAL KIZA BYAMUNGU. 

 

/sites/default/files/2025-11/05112025-p-s-journalswahilimatin-00web_0.mp3