journal matin

Habari zetu za Jumatano tarehe 19 november 2025.

  • -Félix Tshisekedi azindua jedwali la pande zote kuhusu ajira kwa vijana na ujasiriamali
  • -Kinshasa: Martin Fayulu atoa wito wa mazungumzo
  • -Bukavu: Hakuna usaidizi kwa watu waliohamishwa makazi yao, mapigano huko Buhini, na SOS kutoka Mashirika ya Kiraia.
  • -Goma: Mgogoro wa kibinadamu kaskazini mwa Bwito na SOS kutoka Mashirika ya Kiraia
  • -Kananga: Ziara ya mkurugenzi wa eneo wa UNHCR ili kutoa usaidizi kwa waliorejea kutoka Angola
  • -Kinshasa: Ukaguzi wa vibali utaanza Jumano
  • -Lubumbashi: Ufuatiliaji wa ajali ya ndege na matokeo kutoka kwa ofisi ya uchunguzi
  • -Beni: Tahadhari kuhusu maji ya kunywa yasiyo salama katika wilaya ya Ishasa

2er partie:

MGENI

Kampuni ya uchimbaji madini ya Punia Kasese MINING (PKM) bado haija weza kuzindua uchimbaji madini wa ki industria katika eneo la Punia. Zaidi ya hayo, kuna onekana pia kutoku heshimu kanuni za uchimbaji madini katika enneo hilo. Kampuni hiyo inapaza sauti na kutoa wito kwa viongozi kurejesha utulivu katika sekta ya madini. ELOI BUNDIBULYA BUGOYE, mwanasheria wa Punia Kasese MINING (PKM), anajadili hili na Florence KIZA LUNGA.

RIPOTI MAALUM

Mjini Goma, angalau wanawake vijana 75, waundaji wa chapa mpya za nguo, walikamilisha mafunzo yao kunapita siku chache. Mafunzo ilizotolewa na kampuni ya "Alinda House Fashion Academy." Vijana hawa  sasa wako tayari kuanza kuunda mitindo mpya ya mavazi hasa, mitindo ya Kikongo "iliyotengenezwa nchini DRC". Wageni wengi wali huzuria sherehe ya kukomesha mafunzo haya. Bernardine Diambu Alitunadalia Ripoti.

/sites/default/files/2025-11/19112025-journalswahilimatin-00web.mp3