Habari zetu za Jumatano tarehe 3 disember 2025.
- -Beni: Zaidi ya maafisa wa polisi elfu moja wametumwa hadi Oicha, mji mkuu wa eneo la Beni, ili kuimarisha usalama katika maeneo ya kilimo kabla ya likizo.
- -Goma: Hali ya wasiwasi na hofu katika eneo la Ufamandu 2 baada ya makabiliano kati ya makundi mawili ya wanamgambo wa Wazalendo.
- -Bunia: Kutoweka kwa watendaji wa mashirika ya kiraia na wasiwasi miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu.
- -Kinshasa: Serikali yatangaza mwisho wa janga la Ebola/
- -Kananga: Maoni kutoka kwa chifu wa Bulape.
- -Kananga: Maoni kutoka kwa mratibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Umma/
- -Mbujimayi: Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula yuko Ngandajika kuzindua ujenzi wa barabara za kuingia katika Hifadhi ya Kilimo ya Ngandajika.
- -Lubumbashi: Matukio kadhaa yameripotiwa mjini humo yakihusisha baadhi ya askari wa trafiki wanaotuhumiwa kuwashambulia madereva.
2eme partie.
Mgeni:
Mji wa Beni ulipokea toleo la kwanza la Tamasha la Vitabu na Sanaa kuanzia tarehe 28 hadi 30 novemba. Tukio hili la kitamaduni limeandaliwa na shirika la uchapishaji "NGE" kwa ushirikiano na EUNIC-DRC. Je, ni mambo gani muhimu ya kuchukua kutoka kwa tukio hili na malengo yake ni nini? Tulizungumza na afisa wake wa mawasiliano, Ramessou Kabyona, katika mahojiano haya na Marc Maro Fimbo.
Ripoti Maalum
Katika jimbo la Maniema, kampeni ya kutunza fistula kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Kindu inaendelea vizuri. Kati ya wanawake 70 wenye ugonjwa wa fistula wanaotarajiwa kutibiwa, takriban kumi wamesha Tunzwa, na wengine wanasubiri. Florence KIZA LUNGA alitembelea hospitali ya jimbo ambapo taratibu hizo zinafanyika na anatuletea ripoti hii.
/sites/default/files/2025-12/031225-p-s-journalswahilimatin-00web.mp3



