Habari za siku ya pili jioni tarehe 16/01/2024
- Siku ya pili hii tarehe kumi na sita mwezi wa kwanza mwaka hu tunao inchi ya Kongo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka makumi mawili na tatu ya kuuawa kwa Mzee Laurent-Desiré Kabila.
- Kuhusu tu kumbukumbu ya miaka makumi miwili na tatu tangu Mzée Laurent Desiré Kabila kuuawawa katika offisi yake hapa mjini hapa mjini Kinshasa. Ibada ya shukrani Kwa Mungu iliandaliwa siku ya pili hii na shirika Fondation Laurent-Desire Kabila katika Kanisa Kuu la CentenaireProtestant ya mtaa wa Lingwala.
- Msimamizi wa Offisi ya Uchaguzi CENI mjini Kikwit katika jimbo la Kwilu amesimamishwa kazini na viongozi wake.
- Huko Jimboni Ituri, mkusanyiko wa jamii katika eneo la Irumu unahimiza vyama vya kisiasa vinaviopinga matoekeyo ya uchagzu ya wanabunge kwenda ku mahakama ya kikatiba.
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini, zaidi ya familia mia mbili zimelala indje kwa zaidi ya wiki mbili katika mtaa wa Shabunda.
- Jimboni Kwilu, tarafa ya mazingira ya mkoa inasema imeona siku hizi kuongezeka kwa maji katika mito kadhaa na vijito vingine katika jimbo hilo.
- Tatizo la maji ya kunywa huko Mbuji-Mayi huko Kasai-Oriental. Vitongoji kadhaa vinavyotumiwa na shirika REGIDESO huko Mbuji Mayi vimekosa maji kwa karibu wiki moja.
- Kombe la Mataifa ya Afrika Huko inchini Cote d’Ivoire. Inchi ya Kongo yakidemokratia itacheza mechi yake ya kwanza siku ya tatu hii na inchi ya Zambia. /sites/default/files/2024-01/160124-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3




