Habari za jioni 27 Januari, 2025
- Goma : Hali ya usalama katika mji wa Goma bado ni ya kuchanganyikiwa na ya wasiwasi huko Kivu Kaskazini baada ya kuingiya mjini kwa waasi wa M23 kuripotiwa. Viongozi wa Kongo wanaita wakazi kwa utulivu wakihakikishia kwamba hatua zinachulukilwa ili kuwatimua waasi hao wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda.
- Kinshasa : Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), William Ruto anatangaza mkutano usio wa kawaida wa EAC kuhusu hali ya usalama inayoendelea inchini Kongo.
- Mbuji Mayi : Shirika la Maendeleo la Ubelgiji ENABEL lilizindua mradi mpya wa Kupunguza Uzalishaji wa hewa mbaya kutokana na Ukataji miti na Uharibifu wa Ardhi Siku ya tano iliyopita ambao utatekelezwa katika majimbo ya Kasai Oriental na Lomami./sites/default/files/2025-01/270125-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3