Journal Soir

Habari za jioni 28 Mei, 2025

  • Bunia: Mazungumzo kati ya jamii za wa Hema na wa Lendu yalianza hii Siku ya tatu tarehe makumi mbili na nane Mei huko Fataki katika tarafa la Djugu, jimboni Ituri. Lengo ni kupunguza mivutano kati yao  
  • Kinshasa: Mchakato wa kupata pasipoti mpya ya kibayometriki utaanza Siku ya ine tarehe tano Juni mwaka huu. Waziri wa Mambo ya Nje, Thérèse Kayikwamba Wagner, anasema kwamba kuzindua pasipoti hii mpya ni matarajio katika kukabiliana na mabadiliko ya viwango vya kimataifa
  • Matadi: Jimboni Kongo centrale, Wakaazi wa tabaka Nkolo, tarafa la Mbanza Ngungu wanakabiliwa na uvamizi wa vipepeo ambao wanaruka hewani na kuweka mayai kwenye mashamba ya eneo hili. Wanaofia kuharibiwa kwa mimea na vipepeo hao./sites/default/files/2025-05/280525-p-s-journalswahilisoir-00-web_0.mp3