Habari za jioni 09 Juni, 2025
- Kinshasa : Mpango wa serikali ya Kongo wa kuzaa hospitalini bila malipo umeleta utata inchini. Vituo vingi vya afya vinavyotekeleza mpango huo vimeusimamisha vikidai kwamba havijalipwa tangu miezi kadhaa kwa ajili hiyo
- Kinshasa : Serikali ya Kongo inatoa onyo dhidi ya wale wote wanaokosesha usalama mjini Kinshasa. Naibu Waziri wa Sheria na Mashauri ya Kimataifa, Samuel Mbemba wamesema hayo hii siku ya kwanza wakati wa mkutano na waandishi wa habari
- Goma: Huko Kivu Kaskazini, walimu wa tarafa la Masisi wanadai mishahara yao ya miezi mitano tangu mwezi Januari iliyopita. Wanailaumu Caritas, wakala wa kulipa, na wanatishia kuanzisha mgomo./sites/default/files/2025-06/090625-p-s-journalswahilisoir-00-web_2.mp3