Journal Soir

Habari ya jioni 19 Juni, 2025

  • KINSHASA: Wataalamu wa Kongo na Rwanda walianzisha hati ya maandalizi ya makubaliano ya amani hii Siku ya tatu tarehe kumi na nane Juni mwaka tunao, mjini Washington, chini ya upatanishi wa Marekani. Ni Hatua nyingine kuelekea amani mashariki mwa Kongo
  • KINSHASA : Mjini Kinshasa, Waziri wa Sheria Constant Mutamba aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mkuu wa Nchi, siku tatu baada ya Bunge la Kitaifa kuruhusu kufunguliwa mashtaka dhidi yake. Katika barua yake, alishutumu kile anachokiita njama ya kisiasa "iliyoandaliwa mjini Kigali" kwa lengo la kupunguza kasi ya mapambano yake dhidi ya AFC/M23
  • KINSHASA : Shule ya Kitaifa ya Utawala (ENA) ilitia saini mkataba wa ushirikiano na Timu ya Mradi ya Wizara ya Fedha hii siku ya ine mjini Kinshasa. Ushirikiano huu unahusisha kutoa mafunzo kwa zaidi ya wafanyakazi wake./sites/default/files/2025-06/190625-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3