Journal Soir

Habari za jioni 20 Juni, 2025

  • Bunia : Wanamgambo wanne kutoka kundi la wapiganaji la Convention pour la Revolution Populaire, CRP kwa kifupi, waliuawa na wanajeshi sita walijeruhiwa hii siku ya ine katika kijiji cha TSIKU tarafani Djugu huko Itruri. Ilikuwa wakati wa mapigano kati ya wanamgambo wa Thomas LUBANGA na jeshi la  FARDC
  • Goma : Katika Kivu Kaskazini, angalau miili kumi na saba ilitolewa kwenye shimo la eneo la uchimbaji madini la Bibatama, DD3, kutokana na maporomoko ya udongo hii siku ya ine. Kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani, miili iliyo karibu pekee ndiyo iliweza kupatikana
  • Kinshasa : Mjini Kinshasa, Mhariri mkuu wa kwanza kabisa Mkongo wa Redio Okapi Leonard Mulamba Kalala, ambaye alifariki tarehe tano juni mwaka tunao  alipelekwa kwenye mapumziko yake ya mwisho hii siku ya tano tarehe makumi mbili. Katika idhaa hii, tunakupa ushuhuda wa mwanahabari wetu Jean Desire Kanyama/sites/default/files/2025-06/200625-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3