Habari zetu za jumatano tarehe 24 julay 2025
- Mjini kinshasa Mahakama ya Cassation inakataa pingamizi zote vya upande wa utetezi wake waziri wa zamani wa sheria Constant Mutamba. Mahakama hii Imetoka tu kutoa uamuzi wake wa awali. hakuna kifungu cha sheria kilichokiukwa na haijisikii kufungwa na hatua zilizochukuliwa Bungeni.
- Baraza la Kitaifa la Kufuatilia Mkataba na Mchakato wa Uchaguzi, CNSA, linatoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo ya kina na jumuishi. CNSA ilikaribisha kutiwa saini kwa mkataba huo kimsingi kati ya Serikali na AFC/M23, na kuuita "ramani iliyo wazi" kuelekea amani ya kina.
- katika jimbo la Lomami..Dactari Sylvain Muanda anawaomba wakazi kuchemsha maji ya chemchemu kabla ya kuyatumia.Idadi kubwa ya kesi za kipindupindu zimehesabika katika eneo la afya la Ngandanjika, tangu Februari mwaka jana..
/sites/default/files/2025-07/230725-p-s-journalswahilisoir-00web.mp3