Habari zetu za Jumatatu september 08.
- Hali ya usalama mjini Uvira inaelendeleya kuwa ya wasisi. Maelfu ya wakaazi waliandamana Jumatatu ili kuomba Jemadari Olivier Gasita aondoke. Angalau watu wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa vurugo hili.
- Kasai mashariki, SYNAMED Muungano wa Kitaifa wa Madaktari, wanadai malipo halisi na kwa wakati wa mishahara yao. SYNAMED likashifu unyanyasaji unao tendewa kwao na serikali kuu. Na ilitoa makataa ya saa 48 kwa serikali kuboresha hali ya malipo.
- Huko Ituri: karibu tani elfu 35 za kakao tayari zimesafirishwa kwa njia ya kimagendo nje ya jimbo hadi Uganda . Hayo yalitangazwa Jumamosi iliyopita mjini Bunia na Waziri wa Kilimo, Muhindo Nzangi, ambako alijadili kampeni ya kilimo ya 2025-2026.
/sites/default/files/2025-09/08092025-journaswahilisoir-00web.mp3








