Habari zetu za Jumanne tarehe 16 septemba
- Maniema, bei ya vyakula, hasa zaidi mboga kutoka vijiji jirani inapanda mnara tangu siku chache. Wafanyabiashara wanawake, kwa upande wao, wanaongeza bei ya mboga ili kupata faida. Wakaaji wanatoa wito kwa mamlaka kuleta msaada katika kutafuta suluhu ya hali hii.
-
Kuhusu afia: Mlipuko wa Ebola unaonekana huko Bulape, Wilaya ya Mweka, Mkoa wa Kasai. Wizara ya Afya ilianza kutoa chanjo kwa wafanyikazi wa afya .Waziri wa afia alitangaza taarifa kuhusu hali ya Ebola, Mpox, na magonjwa ya kipindupindu nchini DRC.
- Tanganyika, shughuli za shule zilianza tena Jumanne hii katika Taasisi ya Mulembwe na Shule ya Msingi ya Kisakala katika eneo la Moba. Wafanyakazi waliojenga shule hizo katika mradi wa PDL-145 wamekuwa wakifunga milango ya madarasa kwa wiki mbili kwakudai malipo ya mishahara yao kutoka kwa kampuni ya SAFRICAS.
/sites/default/files/2025-09/16092025-journalswahilisoir-00web.mp3






