journal soir

Habari zetu za Jumatatu tarehe 20 september 

  • Polisi wa kijeshi wanakuja kusaidia polisi wa trafiki kwenye barabara fulani za Kinshasa. Hawa wametumwa kupunguza msongamano wa magari. Wanaonekana hapo Kintambo Magasin na Socimat, na pia kwenye mzunguko wa Huilerie,
  • Mtaani Walikale,  eneo la afya la Kibua, linakabiliwa na matatizo ya kuendesha matunzo. Sababu ni kutokana na uhaba wa dawa muhimu katika maeneo zake 20 za afya .Mganga Mkuu wa eneo la afya la Kibua anatuma mwito wakuomba kusaidiwa na washirika piya viongozi wa afya.
  • Mjini Lubumbashi, baadhi ya viwanda vya kutengeneza mikate vinazalisha mkate katika mazingira machafu. Viongozi wa jiji hilo waliamuru  kufunga maduka haya ya mkate kwa kushindwa kufuata hatua za usafi.

/sites/default/files/2025-09/290925-p-s-journalswahilisoir-00web.mp3