journal soir

Habari zetu za Jumatatu tarehe 5 november 2025.

  • -Kinshasa: Waziri wa Afya atangaza uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya surua katika mikoa
  • -Bukavu: Milipuko katika Kivu Kusini
  • -Mbuji-Mayi: Kuzuka upya kwa Surua katika baadhi ya maeneo ya afya
  • -Lubumbashi: Bonde la asidi katika kampuni ya uchimbaji madini ya CDN limeporomoka, hatari ya uchafuzi wa mazingira
  • -Kinshasa: Mkutano na waandishi wa habari wa Balozi wa Umoja wa Ulaya katika eneo la Maziwa Makuu
  • -Goma: Mtu mashuhuri kutoka eneo la Rutshuru aomba uingiliaji kati wa dharura wa kibinadamu
  • -Bukavu: Kufungwa kwa kudumu kwa eneo la uchimbaji madini la Lomer
  • -Kinshasa: Vipi kuhusu kucheleweshwa kwa mapitio ya bajeti katika Bunge la Kitaifa?

2er partie:

Mwaliwa : Bukavu : Shirikisho lenye lengo la kuendelesha urirhi wa hayati Askofu Christophe Munzihirwa, kupitia kuwahimiza watu kuishi pamoja kwa amani kati ya jamii, ilizinduliwa huko Bukavu tarehe 29 Oktoba, kumbukumbu ya miaka 29 ya kuuawa kwa askofu na askari wa AFDL. Mpango huu, unaoitwa Muungano wa Wananchi wa Mabadiliko ya Kijamii, ulifanya mkutano wa video na wanachama huko Goma, Kinshasa, Lyon (Ufaransa), na Brussels (Ubelgiji). Mratibu wa mpango huu ni Bi Alliance Heri, ambaye ni mgeni wetu akizungumza na Jean Kasami.

 Ripoti : Jimboni Ituri, takriban watu mia moja, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, walipata huduma ya afya ya bure mjini Bunia siku ya ine iliyo pita. Hii ilifanyika wakati wa kampeni ya matibabu ya bure iliyoandaliwa na askari wa Monusco toka nchin ya Bangladesh. Lengo ni kuwalinda watu hawa kupitia huduma bora za afya. Ripoti MARTIAL KIZA BYAMUNGU.

/sites/default/files/2025-11/05112025-p-s-journalswahilisoir-00web_0.mp3