journal soir

Habari zetu za Jumatano tarehe 19 november 2025.

  • -Kananga: Takriban watu sitini wamekufa kufuatia kuzama kwa boti ya nyangumi huko Ilebo
  • -Kinshasa: Matatizo ya usafiri kutokana na leseni ya udereva na ukaguzi wa ukaguzi wa gari
  • -Kinshasa: Ufunguzi wa Kikao cha 84 cha Kamati Tendaji ya Umoja wa Mabunge ya Afrika
  • -Kinshasa: Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2026 ulitangazwa kuwa unakubalika na Bunge
  • -Mbandaka: Kuondolewa kwa Makamu Gavana wa Mkoa wa Mongala
  • -Kinshasa: Mkutano kati ya Félix Tshisekedi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kanda ya Maziwa Makuu, Huang Xia/Muhtasari
  • -Beni: Kampeni ya uhamasishaji dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.
  • -Goma: Matatizo ya uendeshaji katika shule 3 kufuatia Mvua.
  • -Mbujimayi: Tani 140 za mahindi zinauzwa Lomami.

2er partie:

MGENI

Kampuni ya uchimbaji madini ya Punia Kasese MINING (PKM) bado haija weza kuzindua uchimbaji madini wa ki industria katika eneo la Punia. Zaidi ya hayo, kuna onekana pia kutoku heshimu kanuni za uchimbaji madini katika enneo hilo. Kampuni hiyo inapaza sauti na kutoa wito kwa viongozi kurejesha utulivu katika sekta ya madini. ELOI BUNDIBULYA BUGOYE, mwanasheria wa Punia Kasese MINING (PKM), anajadili hili na Florence KIZA LUNGA.

RIPOTI MAALUM

Mjini Goma, angalau wanawake vijana 75, waundaji wa chapa mpya za nguo, walikamilisha mafunzo yao kunapita siku chache. Mafunzo ilizotolewa na kampuni ya "Alinda House Fashion Academy." Vijana hawa  sasa wako tayari kuanza kuunda mitindo mpya ya mavazi hasa, mitindo ya Kikongo "iliyotengenezwa nchini DRC". Wageni wengi wali huzuria sherehe ya kukomesha mafunzo haya. Bernardine Diambu Alitunadalia Ripoti.

/sites/default/files/2025-11/19112025-journalswahilisoir-00web.mp3