journal soir

Habari zetu za Alhamisi tarehe 20 november 2025.

 

  • -Kinshasa: Taarifa mpya kuhusu ziara ya Mkurugenzi wa Kanda ya UNHCR nchini DRC na taarifa yake ya SIOS kwa wafadhili
  • -Beni: Wanachama wanawake wa vyama vya wanawake wanashutumu ongezeko la mashambulizi ya ADF dhidi ya raia.
  • -Goma: Siku ya Kimataifa ya Haki za Watoto, Novemba 20.
  • -Kinshasa: Waziri Mkuu yuko Geneva kwa misheni inayoangazia ufuatiliaji wa madini.
  • -Kinshasa: Kuwasili kwa Amiri wa Qatar na Makubaliano ya kuimarisha mikataba iliyopo.
  • -Bunia: Walimu 500 wanawatelekeza wanafunzi wao kwa ajili ya kuchimba dhahabu.
  • -Bukavu: Nyumba 1,500 zimeharibiwa Ishasa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
  • -Lubumbashi: Msemaji wa polisi wa Haut-Katanga kuhusu kuwalinda wakazi wa Kalemie katika maandalizi ya likizo za mwisho wa mwaka wa Mwaka.
  • -Sports: Leopards wanawajua wapinzani wao kwa Kombe la Dunia la 2026/

 

  • 2er partie:

    Mgeni 

    Katika mji wa Beni, visa 55 vya moto vilipelekea nyumba kuungua  na takriban vifo 10 vimerekodiwa na huduma ya Ulinzi wa Raia tangu Januari. Usimamizi mbovu wa moto wa kupikia na uwekaji umeme duni ndio sababu kuu za moto huu. Ni tabia gani Wakaaji wana ombwa kua nayo ili kupunguza visa hivi?   Tunajadili hili na mratibu wa Ulinzi wa Raia wa eneo la Beni. Jean-Paul Kapitula akiongea na Marc Maro Fimbo.

    Ripoti Maalum 

    Katika jimbo la Maniema, Mtandao wa Mashirika ya Maendeleo ya Jamii, unaofadhiliwa na Action Aid International DRC, unasaidia jamii 1,350 zilizoathiriwa na mvua kubwa na upepo mkali wa tarehe 26 Agosti. Msaada ya shirika hilo inakuwemo fedha, ikiwa ni dola za marekani 111.90 kwa kila jamii. Zaidia ya pesa, jamii zinapokea pia  vifaa vya usafi, na vifaa vya shule kwa wanafunzi 900 katika eneo la Kibombo. Msaada huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa "Msaada wa sekta nyingi kwa watu walioathirika na upepo mkali katika mji wa Kindu na maeneo jirani." Florence KIZA LUNGA ndiye aliyeandika ripoti hii.

/sites/default/files/2025-11/20112025-journalswahilisoir-00web.mp3