Habari zetu za Jumatatu tarehe 24 november 2025.
- -Bukavu: Takriban watu hamsini wamekufa kufuatia mashua kupinduka kwenye Ziwa Tanganyika
- -Beni: Watu watano walionusurika katika ajali ya meli kwenye Mto Semuliki
- -Kinshasa: Mkutano wa EU-AU mjini Luanda: Matarajio mapya ya ushirikiano wa Ulaya na Afrika
- -Bunia: Watu 20 waliohamishwa wamezuiliwa baada ya upekuzi
- -Kalemie: Wakaazi wa kijiji cha Musebe huko Nyunzu wanamtuhumu Wazalendo wanaodaiwa kuwanyanyasa
- -Matadi: Ukosefu wa maji ya kunywa Mpozi.
- -Kindu: Mradi wa kuwawekea umeme wodi za wazazi, vituo vya afya na hospital
- -Kinshasa: Mapendekezo ya Waziri Samuel Mbemba kuhusu haki za wafanyakazi
2er partie:
Mgeni:
Wahami wa Burhinyi, katika mtaa wa Mwenga, wanapitia wakati mgumu kutokana na familia zinazowapokea ambao pia zinashindwa kujibu kwa mahitaji yao wenyewe ya msingi. Vikosi vyote vinavyofanya kazi huko Burhinyi vinatuma SOS kwa niaba ya watu hawa wanaoteseka. Riziki Cizungu, presidenti wa jumuiya ya kiraia ya Burhinyi, ndiye mgeni wetu. Anajadili hali ya watu hawa waliohamishwa kwa undani katika mahojiano haya na Jean Kasami…
Ripoti Maalum:
Kuimarisha ushiriki wa kisiasa wa wanawake na vijana katika ngazi ya chini ili kukuza uongozi mpya katika jimbo la Maniema. Hili ndilo lengo linalofuatiliwa na Mfumo wa Kudumu wa Ushauri wa Wanawake wa Kongo (CAFCO). Terehe 18 novemba, siku ya kutafakari ilifanyika ili kutathmini maendeleo na changamoto za ushiriki wa wanawake nchini DRC, na kuelezea matarajio ya siku za usoni kuelekea uchaguzi wa 2028. Wanasiasa kadhaa wa kike na vijana walishiriki katika zoezi hili la kidemokrasia. Maelezo zaidi kutoka kwa Florence Kiza Lunga.
/sites/default/files/2025-11/24112025-swahilijournalsoir-00web.mp3







