journal soir

Habari zetu za Jumatatu  tarehe 1 disemba 2025.

  • -Matadi: Familia 280 za wavuvi zinateseka tangu kunyang'anywa vifaa vyao vya uvuvi.
  • -Bunia: Kuporomoka kwa daraja la Nizi na matokeo yake.
  • -Kananga: Lucha na kampeni ya Salongo.
  • -Beni: Siku ya UKIMWI Duniani, PNLS inahimiza watu wanaoishi na VVU kutumia dawa za kupunguza makali ya VV.
  • -Kisangani: Siku ya UKIMWI Duniani.
  • -Mbujimayi: Uzinduzi wa shughuli za mfuko wa bima ya afya ya walimu ulioidhinishwa.
  • -Kinshasa: Unyanyasaji wa wasichana wanaoendesha pikipiki.
  • -Kinshasa: Zaidi ya madawati 200 yasambazwa kwa shule za umma Kwango.

2eme partie.

Mgeni wetu ni kiongozi wa kijiji cha Yasongo, kilichoko kilomita 73 kutoka Kisangani katika mtaa wa Opala. Hivi majuzi alishiriki katika kikao cha upatanisho na ufafanuzi kati ya sekta ya Yalikandja Yanonge ya Isangi na sekta ya Lobaie katika mtaa wa Opala. Ana zungumzia kazi za wakaaji katika eneo hilo, na hasa, ugumu wa kusafirisha bidhaa za kilimo. Anazungumza na Jacques Mukonkole.

Ripoti maalum.

Siku ya Kimataifa ya Haki za Watoto iliadhimishwa tarehe 20 Novemba. Huko Beni, Kivu Kaskazini, takriban watoto mia moja kutoka shule mbalimbali mjini  walijifunza kuhusu haki zao. Maswali kadhaa kuhusu haki zao yaliulizwa kwa waandalizi wa sherehe hii, pamoja na mapendekezo yao. Marc maro Fimbo atuletea maoni yao mbalimbali katika kipindi hiki.

 

/sites/default/files/2025-12/011225-p-s-journalswahilisoir-00web_0.mp3