Habari zetu za Jumanne tarehe 2 disember 2025.
- -Beni: Zaidi ya maafisa wa polisi elfu moja wametumwa hadi Oicha, mji mkuu wa eneo la Beni, ili kuimarisha usalama katika maeneo ya kilimo kabla ya likizo.
- -Goma: Hali ya wasiwasi na hofu katika eneo la Ufamandu 2 baada ya makabiliano kati ya makundi mawili ya wanamgambo wa Wazalendo.
- -Bunia: Kutoweka kwa watendaji wa mashirika ya kiraia na wasiwasi miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu.-Kinshasa:
- Serikali yatangaza mwisho wa janga la Ebola/
- -Kananga: Maoni kutoka kwa chifu wa Bulape.
- -Kananga: Maoni kutoka kwa mratibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Umma/
- -Mbujimayi: Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula yuko Ngandajika kuzindua ujenzi wa barabara za kuingia katika Hifadhi ya Kilimo ya Ngandajika.
- -Lubumbashi: Matukio kadhaa yameripotiwa mjini humo yakihusisha baadhi ya askari wa trafiki wanaotuhumiwa kuwashambulia madereva.
2eme partie.
Mgeni
Huko Beni, Kivu Kaskazini, ni katika mazingira gani ilisherekewa mwaka huu Siku ya Kimataifa ya Mkataba wa Haki za Mtoto, inayoadhimishwa kila tarehe 20 Novemba? Tuna mpokea Presidenti wa bunge la watoto mjini Beni. Eloge Bwanakawa ana ongea hapa na Marc Maro Fimbo…
Ripoti maalum
Jamii za Yainyongo-Romee katika eneo la Isangi na zile za sekta ya Lobaie katika eneo la Opala zimefanya amani. Ijumaa iliyopita, walitia saini barua ya upatanisho kuhusu mipaka ya maafikiano ya misitu ya jamii huko Yainyongo. Pia waliahidi kuishi kwa mshikamano baina ya jamii na kuwa macho dhidi ya jambo lolote litakaloweza kuharibu uhusiano wa mababu zao. Nini kilikuwa chanzo cha mivutano kati ya jamii hizo mbili? Na ni maelewano gani yaliyofikiwa? Ripoti ya Jacques Mukonkole…
/sites/default/files/2025-12/021225-p-s-journalswahilisoir-00web.mp3








