Habarib za mangaribi, siku ya ine 160426
- Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka , iko New York kwa wakati huu , ili kushiriki katika mikutano Wa Kundi la Benki ya Dunia , ama Banque Mondiale , na Shirika la Fedha la Kimataifa , ama Fond Monétaire international.
- Jimboni Kivu Kusini, haswa katika eneo la Kabambare, utawala Wa Ninja, unakabiliwa na hali ngumu ya kijamii na kiuchumi, kutokana na ukosefu wa usalama unaoendelea kwenye barabara kuu, inayounganisha utawala Wa Ninja na muji Wa Bukavu.
- Tunapokaribia utshunguzi Wa somo la mwisho la secondari, ama Examens d'État , Wakaguzi wa Kitaifa wa Elimu ya Kitaifa na Uraia Mpya wa Kasai Central 1, wamekataza wanafunzi kuandaa kile kinacho itwa "maquis".
- /sites/default/files/2026-04/160426-journalswahili-jeudisoir-00_web.mp3






