Habari za siku ya tano mangaribi tarehe 270226
- Bi Juliana Amato Lumumba , ambaye ni mtoto wa Patrice Emery Lumumba, waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , ndiye mgombea wa Congo wa katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa, la Francophonie.
- Jimboni Kivu Kaskazini, kwa Mwaka mmoja pekee , watoto wanafunzi zaïdi ya elfu mbili ,mia moja na makumi sita , kutoka shule kumi na ine huko Goma na Sake , Hawa endi tena shuleni .
- Katika eneo la Fizi, mvua kubwa iliyonyesha , Siku ya ine hii iliopita, mwezi tulimo , ilisababisha uharibifu mkubwa wa kibinadamu na nyenzo, katika sekta ya Mutambala, kijiji cha Mukera.
- /sites/default/files/2026-02/270226-journalswahilivendredisoir-web.mp3






