Zaidi ya watoto kumi wamepoteza maisha walipozama Mtoni Lulua, mtaani Demba, jimboni Kasai ya Kati. Ilikuwa wakati mtumbwi waliokuwemo uli pinduka.
Miili ya raia kumi ilipatikana Jumatano, Agusti 5, ndani la kanisa moja kijijini Munguiko. Wahanga hawa waliuwawa katika shambulio linalohusisha waasi wa ADF.
Tuta jielekeza piya majimbo Kasai na Bandundu ambapo Vijana wengi wanakataa kukata tamaa mbele ya changamoto za kimaisha. Wengi wanajipatiya fursa za kiuchumi ili kujisaidiya kimaisha. Tutafata ripoti yake Esther Ndalafina .
/sites/default/files/2026-08/060826-journal-sw-_jeudi_soir.mp3






