Meli iliyo zuiliwa karibu na mji mkuu Kinshasa kwa sababu ya shaka ya kuwepo kwa wagonjwa wa Ebola imeachiliwa baada ya vipimo kutokuonyesha kesi yoyote ya ugonjwa huo. Viongozi wanasema taarifa ya hatari ilitolewa baada ya uchunguzi wa afya kufanyika ndani ya meli.
Gavana wa kijeshi wa Ituri, Jenerali Gaby Kasongo, amefanya ziara yake ya kwanza mtaani Djugu, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukosefu wa usalama. Anatarajiwa kusikiliza wananchi na viongozi mbalimbali kuhusu mahangaiko yao na mapendekezo ya kurejesha amani ya kudumu katika eneo hilo.
/sites/default/files/2026-08/100826-p-s-bloc_complet_journal-00.mp3





