Journal Swahili Matin, 14 Juillet 2026.

Wagonjwa wa Ebola arubaini na mbili wali rikodiwa, miongoni mwao wengine ishirini na ine kupoteza maisha kwa mda wa masaa arubaini na nane. Hii ni ripoti ya chumba cha kazi ya dharura ya matibabu ya kijamii mjini Bunia.

Wafanya kazi wa kampuni ITM Sarl wa huko Kalemie wagoma kazi wakidayi malipo ya maruporupo yao ya miezi kumi na tano. Kampuni ya Safricas imeombwa ku changia swala lile

Na utulivu ume onekana pa Kasake mtaani Masisi na pa Lumbishi mtaani Kalehe kisha mapambano ya siku tatu kati ya wapiganaji Wazalendo na waasi wa AFC-M23. Wakaaji walio kimbia waanza kurudi makwao wamoja kisha wengine.

/sites/default/files/2026-07/140726-journal-swahili-matin-00.mp3